Nteghenjwa Hosseah, Arusha

Wakazi zaidi ya 27,000 wa kata ya Murriet iliyopo Jiji la Arusha wataondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya km 15 kusaka huduma ya Afya na kujifungua kwa akina mama baada ya Mkuu wa wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro kuzindua ujenzi wa Kituo cha Afya kitakachogharimu zaidi ya shilingi milioni 400 katika kata hiyo.

Kuanza kwa ujenzi wa Kituo cha Afya kitakachokuwa cha kisasa ni kufuatia malalamiko ya muda mrefu ya wananchi wa eneo hilo kwa Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa alipokuwa katika ziara Mkoani Arusha hususani katika Jiji la Arusha kuwa kata hiyo yenye wakazi hao haina zahanati wala kituo cha afya cha uhakika na kufikia hatua ya akina mama kujifungulia nyumbani au njiani wakati wakienda katika kituo cha Afya za Levolosi kilichopo umbali wa km 15 .

Kufuatia malalamiko hayo ya akina mama waliokuwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali ya kutaka kituo cha afya au zahanati,Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza mara moja huduma hiyo kuwafikia wananchi bila ya kuchelewa.

Mhe. Daqarro alisema kuanza kwa ujenzi wa kituo hicho ni kufuatia jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mhe. Mrisho Gambo kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi kama vile matofali 3, 000, mifuko ya sementi 100 na bati 100 kwa ajili ya ujenzi huo.
1. Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro akishirkiana na wananchi kuchimba Msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Muriet.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia(mbele) akishiriki kuchimba Msingi wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Muriet.
Wananchi wa Kata ya Muriet wakishiriki katika Ujenzi wa Msingi wa Kituo cha Afya, zoezi la ujenzi limezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...