Dk.
Senkoro aliyegombea urais mwaka 2005 kupitia Chama cha TPP –Maendeleo
alifariki dunia ghafla Januari 4, mwaka huu wakati akipelekwa Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.
Shughuli
ya kumuaga Dk. Senkoro ilianzia leo nyumbani kwake, Tabata Segerea,
kisha mwili wake ulihamishiwa katika Kanisa la Winners Chapel
International, Banana, Ukonga kwa ibada fupi, ambapo viongozi walitoa
salamu za rambirambi.
Mbali
na Makinda, viongozi wengine waliohudhuria ni; Katibu wa Itikadi na
Uenezi CCM, Humphrey Polepole na Mwnyekiti wa Chadema Wilaya ya Ilala,
Dk. Makongoro Mahanga.Akizungumza
baada ya ibada hiyo, Makinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), alisema alipokea kwa mshtuko mkubwa
kifo cha rafiki yake na mdogo wake huyo katika siasa.
Alisema
Dk. Senkoro alijaribu kuwa rais mwaka 2005, lakini Mungu akamwambia
anaweza kuwatumikia wananchi kwa njia nyingine kama alivyofanya.“Tumemuamini
Kristo hivyo hatuwezi kufika kwake bila kulala na Anna amefariki dunia
katika Ukristo, swali, jiulize wewe kama ungekuwa Senkoro ungekwenda
wapi?” alihoji Makinda.
Alisema familia yake ikae kwa amani na kwamba waamini Anna yuko kwa Mungu amekwenda kutuandalia makao.Naye
Dk. Mahanga akitoa salamu za Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na
rafiki yake, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, alisema
wamesikitishwa na kifo hicho na kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki
walioondokewa na kipenzi chao.
"Sisi
kama chama tumempoteza kamanda mwenzetu na mpambanaji toka alipojiunga
na chama mwaka juzi Julai, yote ni mapenzi ya Mungu," alisema Dk.
Mahanga.Kwa
upande wake, Polepole akitoa salamu kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama
hicho, Rais John Magufuli pamoja na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana
alisema:
"Tuishi
maisha mema na yenye kutenda haki kwa sababu Biblia inasema taifa
linalotenda haki Mungu uliinua pamoja na kuwa waaminifu kwa uajibikaji
na kutenda haki."Dk.
Senkoro wakati wa uhai wake aliwahi kufanya kazi katika Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi katika Gereza la Ukonga, ameacha watoto watu na
wajukuu wawili.
Msemaji
wa Taasisi ya JKCI, Maulid Kikondo, alisema mara ya mwisho kabla ya
kufikwa na mauti, Dk. Senkoro alifika hospitalini hapo kwa ajili ya
matibabu na kufanyiwa vipimo kadhaa ambavyo madaktari waligundua tatizo
lililokuwa likimsumbua.
Alisema
jopo la madaktari bingwa wa taasisi hiyo walikuwa na nafasi ya kuokoa
maisha ya Senkoro iwapo angekubali kulazwa kwa ajili ya matibabu katika
kitengo hicho.Alisema baada ya vipimo alishauriwa kulazwa kutokana na hali yake, lakini Dk. Senkoro alikataa na kutaka kurudi nyumbani.
Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa Kwanza Mwanamke marehemu Anna Senkoro katika Kanisa la Wninner Chapels International jijini Dar es Salaam jana, Marehemu alizikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la marehemu Anna Senkoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...