Na Judith Mhina - MAELEZO
Waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, Pili na ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mtaalamu wa lugha ya Kiswahili, Dkt Mohammed Seif Khatibu (pichani) amesema Mapinduzi ya Zanzubar ya mwaka 1964 yalimaliza mateso ya muda mrefu waliyoyapata Waafrika wa Tanzania Bara na Visiwani.

Dkt.  Mohammed Seif Khatibu amesema hayo alipohojiwa na Idara ya Habari - MAELEZO leo kuhusiana na mafanikio yaliyopatikana tangu mapinduzi ya Zanzibar yalipofanyika miaka 53 iliyopita. 
Amesema, Mapinduzi yameondoa madhila ya utumwa, masuria, kubaguliwa, kufanyishwa kazi, kudhalilishwa, kunyanyaswa, kudharauliwa na kuuzwa kama samaki:

“Inashangaza kuona Watanzania hawasheherekei ipasavyo Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa kama si Mapinduzi hayo mateso na madhila kwa Waafrika wa Bara na Visiwani yangeendelea”. “Madhila ya Zanzibar hayawagusi Waafrika wa Zanzibar peke yake, bali pia Waafrika wa Tanzania Bara”. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...