Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inalaani vikali uchochezi unaofanywa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Loliondo na Ngorongoro ya kuwahimiza wananchi kuchunga, kulima na kukata miti katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo hali inayochangia kukausha vyanzo maji yanayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
Akizungumza na Waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema maelfu ya mifugo kutoka nchi jirani ya Kenya imekuwa ikiingizwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti muda wa saa 11 jioni, Amesema katika kukabiliana na changamoto ya uharibu wa chanzo kikuu cha maji ya Serengeti kwa asilimia 47.2 ya maji yote, tayari mifugo 1700 imeshakamatwa Mbali na mifugo hiyo.
Waziri Maghembe alisema kuwa maelfu ya Matrekta ya kutoka nchini Kenya yameletwa kulima katika maeneo yanayopakana na Serengeti Aliongeza kuwa hivi karibuni kilimo kimeshamiri ambapo kipindi cha nyuma wakazi walikuwa wanalima na ng’ombe (maksai) ila sasa matrekta ya Kenya yanalima na kufungua mashamba makubwa.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Maghembe ameagiza kuwa raia wa Kenya wenye mifugo Loliondo warudi makwao mara moja, Mkoa na Wilaya uchukue hatua kuwaondoa mara moja Pia, Matrekta yote ya nchi ya Kenya yawe na usajili wa kodi (Tax Clearance) toka TRA au yarudi kwao mara moja Aidha, ameagiza kuwa eneo la 1,5002km liwekewe alama mara moja na uwekaji alama ukamilike ifikapo tarehe 30 Machi, 2017. 
 Kwa upande wa Utalii, ameziagiza kampuni zote za utalii ambazo hazina usajili wa kitaifa zinazofanya biashara kwa mikataba ya vijiji ziripoti Wizarani ndani ya siku saba, Ikiwa pamoja na kuonyesha usajili wao, kuonyesha vitalu walivyopewa na Serikali pamoja kuiridhisha Serikali kama wanalipa kodi. 
 Awali, akizungumzia kuhusu mgogoro huo wa Pori Tengefu la Loliondo, Waziri Maghembe alisema anatambua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anasimamia mazungumzo ya wadau wote ili kuleta utatuzi wa mgogoro huo. ‘’Nimeambiwa kuwa mwelekeo wa mazungumzo ni mzuri nahimiza mazungumzo yaendelee, lakini nimeona nikingoja hadi mazungumzo hayo yaishe Hifadhi ya Taifa ya Serengeti itakuwa haipo.’’ alisisitiza
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Waandishi wa habari jana  mjini Dodoma,  kuhusiana na  uchochezi unaofanywa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Loliondo na Ngorongoro ya kuwahimiza wananchi kuchunga, kulima na kukata miti katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo hali inayochangia kukausha  vyanzo maji yanayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
Kundi la mifugo likiwa ndani ya Pori Tengefu la Loliondo, karibu kabisa na mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Picha na Lusungu Helela- Maliasili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ukimchekea nyani utavuna mabua.....kazana Magembe wwaondoke

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...