Na Woinde Shizza,Arusha

Wakuu wa mashirika umeme kutoka katika nchi kumi za Afrika zinazozalisha umeme (Eastern Africa Power pool (EAPP) zimekutana jijini arusha kwa malengo ya kujadili mfumo wa usafirishaji wa umeme ikiwa ni pamoja na namna wananchi wao watakavyoweza pata nishati ya umeme kwa urahisi tofauti
na sasa .

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt.Juliana Palangyo alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa mashirika ya umeme katika nchi hizo za Eastern Africa power pool (EAPP) mapema leo.

Palangyo alisema kuwa lengo halisi ni kuweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo nishati ya umeme kwa watumiaji wake kwani kuna uwezekano mkubwa wa nchi zote zilizo kwenye umoja huo. 

Alisema kwa sasa yapo baadhi ya makampuni ambayo yalikuwa yanauza umeme kwa gharama kubwa hasa kwa wananchi ambao hawajapata huduma hiyo ya umeme lakini kupitia umoja huo wataweza kupata nishati hiyo kwa gharama nafuu.  "Hizi nchi za eastern tumekutana hapa ili tujadili namna ambayo tunaayo wanayoweza kutafuta namna ya kuzalisha umeme kwa bei nafuu na kisha nchi hiyo itaweza kuuza umeme kwa bei ndogo"aliongeza Palangyo. 

Hata hivyo kwa upande Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Tanesco,Bi Leila  Muhaji alisema kuwa katika mkutano huo pia watajadili namna ambavyo Tanzania itajenga njia ya usafirishaji wa umeme wa njia ya maji ambayo itatoka nchi ya Tanzania kwenda nchini Kenya,Zambia,pamoja na nchi nyingine .

Muhaji alisema kuwa Tanzania itanufaika na ujenzi wa njia hizo hivyo jamiii
itanufaika kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwenye nchi ambazo
zimeeendelea Duniani. 

"Hata hivyo mara baada ya mkutano huo,Wakuu wa nchi zinazozalisha umeme tunatarajia pia kuwepo na wadau wengine ambao ni Mawaziri kutoka nchi zote ambao nao sasa wataweza kuweka mambo sawa ili huduma iweze kumfikia mlengwa"aliongeza Muhaji

Alimalizia kwa kutaja nchi ambazo zina unda umoja huo kuwa ni Tanzania ,Kenya,Uganda ,Rwanda ,Burundi ,Sudan , Dr congo, Ethiopia ,Djbout, Libya pamoja na Egypt.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...