Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Bonde la Ziwa Victoria ambaye pia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi cheti cha shukrani, Bi. Joyce Kasebela baada ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuwa mmoja wa wadhamini wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria lilimalizika jana jijini Mwanza.

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt Leonard Chamuriho (kushoto) akifuatiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki wakishiriki Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria lililomalizika jana jijini Mwanza.
Mwakilishi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo wa Jijini Mwanza, Bi. Dorah Michael (kushoto) akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria jana jijini Mwanza.
ASP Andrew Majaliwa (kulia) akiwa ameshika moja ya vipeperushi vya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), baada ya kupata maelezo kuhusu mazingira kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, lililomalizika jana jijini Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...