Mufti
Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akizungumza mapema leo jijini
Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel
iliyopewa jina la ‘Zantel Madrasa’ ambayo ni mahususi kwa waumini wa
dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata
mafundisho kupitia simu za mkononi ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa
Zantel watakaopenda kutumia huduma hii watatakiwa kupiga simu au kutuma
ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo. (katikati) ni
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Mkuu wa kitengo cha huduma na
bidhaa Zantel Hamza Zuheri.
Mkurugenzi
Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza leo jijini Dar es salaam
katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel iliyopewa jina la
‘Zantel Madrasa’ ambayo itawawezesha waumini wa dini ya Kiislamu
kujifunza kuhusu imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia
simu zao za mkononi. (Katikati) ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Aboubakar Zubeiry ambaye alikuwa mgeni rasmi na Mkuu wa Itifaki BAKWATA
Mohammed Nassor.
Mufti
Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel
Benoit Janin wakionyesha vipeperushi vya huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’
kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma hiyo uliofanyika mapema leo jijini
Dar es salaam.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...