Na Karama Kenyunko, 
Globu ya jamii
Baada ya kusota rumande kwa takribani siku saba, hatimae Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji jana amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam kujibu tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya.
Manji ambae pia ni Diwani wa Mbagala Kuu na mfanyabiashara maarufu ameshtakiwa chini ya kifungu cha sheria namba 17(1)(a) ya sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015. Amesomewa mashtaka yake leo na karani wa mahakama hiyo, Sarah Mulokozi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha.
Manji amekananusha kutumia dawa za kulevya na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kuweka dhamana ya milioni kumi na mdhamini mmoja ambaye nae ameweka kiasi hicho hicho cha dhamana.
Manji alifika mahakamani hapo saa nane kasoro nne na alipandishwa mahakamani majira ya saa tisa. Katibu wa klabu hiyo, Charles Boniphace Mkwasa ndiye aliyemuwekea dhamana Manji na kumfanya awe huru.

Katika kesi hiyo Manji anatetewa na mawakili watatu waliokuwa wakiongozwa na wakili Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Jeremiah Mtobesya huku upande wa Jamuhuri ukiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa mashtaka, Oswald Tibabyekomya aliyekuwa akisaidiana na wakili wa serikali Shadrack Kimaro.
Akisoma hati ya mashtaka, Mulokozi amesema kuwa, kati ya Februari 6 na 9 mwaka huu huko Upanga Sea View ndani ya Wilaya ya Ilala jijiini hapa, mshtakiwa alitumia dawa za kulevya aina ya Heroine (diacefyl Morphine)..

Mara baada ya kutimiza masharti ya dhamana Manji aliondoka katika viwanja vya mahakama hiyo akiwa katika gari aina ya Hummer lenye namba za usajili T 670 BBX huku akisindikizwa na umati wa mashabiki wa Yanga.
 Mfanyabiashara Maarufu na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga SC, Yusuf Manji akifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salam.

 Katibu mkuu wa Yangu, Boniface Mkwasa akiwa katika Mahakama ya Kisutu.
Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yangu Clement Sanga akiteta jambo na mmoja wa Mawakili wanaomtetea Yussuf Manji, Alex Mgongolwa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...