Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Bohari Kuu ya Madawa Tanzania (MSD), Cosmas Aron Mwaifani amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kuisababisha kampuni ya H.H Hillal kupata manufaa ya zaidi ya shilingi milioni mia nne.

Mwaifani anashtakiwa pamoja na aliyekuwa Meneja Manunuzi wa MSD Fredrick Rubanga Nicolous.

Mbele ya Hakimu Mkazi Respicius Mwijage, wakili wa serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leornad Swai akisaidiana na Aneth Mavika alidai kuwa washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi  1 hadi 19 mwaka 2013 huko katika makao makuu ya MSD  yaliyopo Temeke jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa siku ya tukio washtakiwa hao wote kwa pamoja wakiwa waajiriwa wa MSD walitumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa na kufanya mabadaliko ya mkataba namba 1 yenye kumbukumbu namba MSD/003/Q/G/2010/2011/60 wa Machi 1, 2013 na kuitisha nambambili wenye kumbu kumbu namba kama hiyo wa Machi 19,mwaka 2013.

Wakili Mavika amesema kuwa kitendo hicho kiliisababisha kampuni ya H.H Hillal kupata manufaa yasiyokuwa ya halali ya Shilingi 482,266,000/.

Washtwakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wako nje kwa dhmana baada ya kukidhi masharti ya dhamana waliyopewana mahakama iliyowataka kuwa na mdhamini mmoja kila mmmoja mwenye barua kutoa serikalini au taasisi yoyote inayotambulika na atakayeweka dhamana ya milioni 20.

Aidha mahakama imewataka washtakiwa hao kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika isiyopungua thamani ya shilingi milioni 200.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21, Mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuwasomewa washtakiwa maelezo ya awali, kwa mujibu wa wakili Swai upelelezi umekamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...