Na.Vero Ignatus ,Arusha.

Mtu moja ambaye jina lake hajijafahamika ameuawa na wananchi wenye hasira kali huko maeneo ya kwa Mrombo Jijini Arusha, akidhaniwa kuwa ni mwizi wa pikipiki baada ya mtu huyo kupita na kufananishwa na waendesha pikipiki hao.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa majira ya saa saba mchana wananchi hao walimuona mtu huyo wakadhania kuwa ndiye aliyewahi kumnyanyanya mwenzao pikipiki hivyo wakaanza kumshambulia na kumburuza ambapo hadi jeshi la polisi kufika eneo la tukio mtu huyo alikuwa tayari ameshachoka na hali yake ilikuwa mbaya wakiwa njiani kumpeleka hospitali alifariki.

Kamanda Charles Mkumbo amewataka wananchi kutochukua sheria mkononi kwani wanaweza kumdhuru mtu ambaye hausiki na tukio amesema kuwa wanapomuhisi mtu kuwa ni muhalifu watoe taarifa kwa jeshi la polisi ili sheria ichukue mkondo wake. 

Hadi sasa jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu watano ambao ni waendesha pikipiki kwa kuhusika katika tukio hilo,mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya maountmeru ukisubiria ndugu na jamaa kwenda kumtambua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...