Na Veronica Simba – Mwanza.

Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, ameanza ziara ya kazi ya takriban juma moja katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali za sekta hiyo.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, Agosti 28 mwaka huu, Kamishna Mchwampaka alikutana na kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Madini, Kanda ya Ziwa Viktoria-Magharibi pamoja na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Ukaguzi wa Madini Kanda ya Mwanza, iliyokuwa ikijulikana kama Wakala wa Ukaguzi Madini Tanzania (TMAA).
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi hizo mbili, Kamishna Mchwampaka aliwataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwaletea wananchi wake maendeleo ya dhati.
Katika hatua nyingine, akizuru Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Kamishna Mchwampaka, alipongeza jitihada za watendaji wa Mradi huo unaomilikiwa na wazawa wazalendo kwa asilimia mia moja, kwa ubia kati ya Isinka Federation 2014 Mining Cooperative Society Limited na Kampuni ya kitanzania ya Busolwa Mining Limited.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (kulia), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Samwel Sweda (wa pili kutoka kushoto), alipofika ofisini kwake akiwa katika ziara ya kazi wilayani humo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Eliud Mwaiteleke. Wengine ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria-Magharibi, Mhandisi Yahya Samamba (kushoto kwa Mkuu wa Wilaya) na Mhandisi Rayson Nkya (wa kwanza kulia).
Mmoja wa Viongozi wa Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Baraka Ezekiel (wa pili kutoka kulia), akifafanua jambo kwa Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) na Ujumbe wake. Kamishna Mchwampaka alitembelea Mradi huo Agosti 28 mwaka huu akiwa katika ziara ya kazi Kanda ya Ziwa 
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati), akiwa ameambatana na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini na wafanyakazi wa Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, wakikagua sehemu mbalimbali za Mgodi huo.


Shughuli za uchimbaji madini zikiendelea katika Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...