Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, Sozi Ngate,(Wapili kulia) akipokea msaada wa kompyuta kati ya 20 toka kwa Mkurugenzi wa Bridge for change,Ocheck Msuva na Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea shule za sekondari ya Kilangala na Miembe Saba,kwaajili ya kuwashauri juu ya mafunzo ya upatikanaji wa masomo kwenye simu za kinganjani na kompyuta(Free Digital Learning) na kutoa msaada wa komyuta kwa kushirikiana na Taasisi ya Bridge for change katika shule hizo mwishoni mwa wiki,Anaeshuhudia kulia ni Mkuu wa shule ya Kilangalanga,Albert Mabiki.
Ofisa Mtambo Tanakilishi wa Vodacom Tanzania PLC, Robert German akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Sekondari ya Kilangalanga iliyopo Mlandizi mkoa wa Pwani wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea shule za sekondari ya Kilangalanga na Miembe Saba,kwa ajili ya kuwashauri kwa juu ya mafunzo ya upatikanaji wa masomo kwenye simu za kinganjani na kompyuta(Free Digital Learning) na kutoa msaada wa kompyuta 20 kwa kushirikiana na Taasisi ya Bridge for change katika shule hizo mwishoni mwa wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...