Na Karama Kenyunko, Blogu ya
jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi
Kisutu imewahukumu watu wa nne kutumikia kifungo cha mika 30 jela na kuchapwa viboko
12, sita wakati wa kuingia na sita wakati wa kutoka baada ya kupatikana na
hatia dhidi ya kosa la wizi wa kutumia silaha.
Hukumu hiyo iliyosomwa na hakimu Mkazi,
Respicious Mwijage imewataja waliofungwa kuwa ni Donald Nzweka, Michael
Pascal,Ally Akili na Kurwa Mwakagenda.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mwijage
amesema, upande wa mashtaka umeweza kuthiitisha kosa hilo pasipo kuacha shaka
na kuwa washtakiwa walishiriki kutenda kosa na kwamba mahakama ilijiuliza
kwamba kosa la kutumia silaha ili lithibitike Jamhuri wana wajibu wa kuthibitisha
bila kuacha shaka kwamba mshtakiwa kabla ya kutenda awe na kifaha hatari au
wawe zaidi ya mmoja na kwamba baada ya tukio hilo walitumia nguvu kwa mtu
waliyeporwa.
Katika kesi hii, mlalamikaji na
mashahidi wengine walieleza kuwa usiku wa julai 7 majambazi walivunja mlango
mkuu wa nyumba yao kwa kutumia bomu ambalo lilitambuliwa na polisi kuwa baruti
na kasha kuendelea kuvunja milango mingine ambapo baada ya hapo waliingia
katika chumba walichokuwa wamekaa, ambacho kilikuwa na mwanga, mshtakiwa mmoja
alishika panga na kuanza kuwapiga kwa
kutumia ubapa.
Amesema, kwa kuzingatia ushahidi
huo hakuna shaka kwamba mashahidi waliweza kuwatambua majambazi na
kuwa utetezi wa washtakiwa kwamba walikamatwa maeneo tofauti na kupelekwa
oysterbay polisi na kupigwa na kunyanyaswa siyo ya kweli.
Kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo,
Hakimu Mwijage aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote na kusema
juu ya washtakiwa ambapo wakili wa serikali Gloria Mwenda, alidai washtakiwa
ni wakosaji wa mara ya kwanza na akaomba
wapewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa jamii.
“Nimeridhika ushahidi wa mashahidi
11 walioletwa na upande wa mashtaka ambao wameweza kuthibitisha bila ya kuacha
shaka kuwa mlitenda kosa, nawahukumu kwenda jela miaka 30 na kuchapwa viboko
12, sita siku mnaingia na sita siku ya kutoka" amesema Mwijage.
Awali ilidaiwa, Julai 7 ,2013 huko
maeneo ya Boko Magengeni, jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao waliiba simu nne
pesa taslimu 150,000 na cheni za dhababu mbili ambapo vitu vyote vina thamani
ya 2050,000 mali ya Hobokela Mwakijambile.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...