Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu amesema kuwa moja ya chanzo kikubwa cha vifo vya akina mama wakati wa kujifungua ni kutokana na kutokwenda kujifungua kwenye vituo vya afya.
Hayo ameyasema leo wakati matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya fedha zitakazosaidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga na kusema sababu kubwa ji ni kukoseakana kwa wataalamu wa kuwahudumia akina mama katika vituo wanapokwenda kujifungua.

Mama Samia amesema ushiriki mkubwa baina ya Amref na serikali katika kuhakikisha wanatoa mafunzo kwa wakunga na mpango huo utasaidia katika kuongeza wataalamu kwenye vituo.

Katika matembez hayo mama Samia ameweza kuwa balozi wa wakunga ikiwa ni baada ya kushiriki kwenye matembezi kwa mara ya pili mfululizo pia ameweza kutoa cheti cha ushiriki kwa makampuni na taasisi mbalimbali.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu akimkabidhi cheti cha ushiriki kwa Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Ushauri wa Kiufundi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya  Dkt Aifena Mramba wakati wa matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya fedha zitakazosaidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu akiwa sambamba na Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee wakiwa katika matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya fedha zitakazosaidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF Florence Temu baada ya kumalizika kwa matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya fedha zitakazosaidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa chama cha wakunga ikiwa ni baada ya kukubali kuwa balozi wa Wakunga.

 Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakionyesha furaha baada ya kumaliza kwa matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya fedha zitakazosaidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.

Wafanyakazi mbalimbali wa asasi za kiraia.
Picha zote na Zainab Nyamka.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...