Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza zoezi la usajili wa watu
katika wilaya zote za mikoa ya Manyara na Singida ambalo linalenga
kuwapatia Vitambulisho vya Taifa.
Kuwapatia Vitambulisho wananchi kutasaidia kutambulika pale wanapotaka kugawiwa pembejeo za Kilimo, kupata leseni za udereva na biashara, kusajili namba za Simu, kumiliki Ardhi, kupata mikopo, kufungua akaunti benki na matumizi mengineyo yanayohitaji utambulisho.
Mratibu wa Usajili wa mikoa ya Manyara na Singida, Thomas William ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara amesema watu wengi wanajitokeza kusajiliwa baada ya kuelimishwa kuhusu umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...