Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi
(katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio
ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais
Dkt. John Pombe Magufuli, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Usajili,
Patrick Kipangula na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Habari na Picha,
Rodney Thadeus.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) wakati akielezea
mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano katika kipindi cha miaka miwili ya
uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli mapema hii leo Jijini Dar es Salaam.Picha
na Idara ya Habari - MAELEZO.
Na
Ismail Ngayonga - MAELEZO
SERIKALI imesema
Tanzania imefanikiwa kupiga hatua kubwa ya maendeleo kutokana na kuimarika kwa
mifumo ya uwekezaji na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika kipindi
cha miaka miwili ya utawala wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), na
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mkutano wake na Waandishi
wa Habari akielezea kuhusu Mafanikio ya miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Alisema
kuwa Mataifa mbalimbali duniani yamekuwa yakiimwagia sifa Serikali ya Awamu ya
Tano kutokana na udhubutu na hatua yake ya kutekeleza miradi mikubwa ya
maendeleo kwa kutumia fedha za ndani, jambo ambalo limeshindwa kutekelezwa na
mataifa mbalimbali ya Bara la Afrika.
Akitolea
mfano Dkt. Abbasi anasema, hadi kufikia sasa Serikali tayari imetenga kiasi cha
shilingi Trilioni 1.9 za mapato yake ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa reli ya
kisasa (SGR) hatua inayolenga kurahisisha shughuli za usafiri pamoja na kuchagiza
shughuli za uchumi na maendeleo ya wananchi.
Dkt.
Abbasi alisema katika kipindi cha miwili ya utawala wa Rais Magufuli, Serikali
ya Awamu ya Tano imefanikiwa kutekeleza ahadi mbalimbali ikiwemo mapambano
dhidi ya rushwa, ufisadi pamoja na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii
ikiwemo elimu, afya, maji umeme na barabara.
“Tangu
kuingia Madarakani, Serikali imeongeza bajeti yake katika sekta muhimu, mfano
katika afya Serikali ya Awamu ya Tano imeongeza bajeti ya dawa na vifaatiba kazi
kutoka Shilingi Bilioni 30 mwaka 2015 hadi Tsh. Bilioni 261 mwaka 2017 pamoja
na kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka Tsh Bilioni
48.6 mwaka 2015 hadi Bilioni 461 mwaka 2017” alisema Dkt. Abbasi.
Anasema
Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuhakikisha kuwa Tanzania inajitegemea
kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa makusanyo wa fedha za ndani,
ambapo katika kipindi cha miaka miwili makusanyo yameweza kuongezeka kutoka
Tsh. Trilioni 9.9 mwaka 2015 hadi Trilioni 14 mwaka 2017.
Aidha
Dkt. Abbasi anasema Serikali ya Awamu ya Tano kuwa imepata mafanikio makubwa
kutokana kupunguza bajeti ya matumizi ya safari kwa Viongozi na Maafisa
kusafiri nje ya nchi kutoka Tsh, Bilioni 216 mwaka 2014/15 hadi kufikia Tsh.
Bilioni 25 kati ya mwaka 2015-17, ambapo fedha hizo zimeweza kutumika katika
kutwekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dkt.
Abbasi anasema katika kutetea na kutekeleza ajenda ya maendeleo kwa wananchi
wake, Serikali ya Awamu ya Tano tayari imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya
madini, ambapo katika mazungumzo yaliyofikiwa hivi karibuni baina ya Serikali
na Kampuni ya Barrick, Serikali itaweza kupata hisa ya asilimia 16 na mgawanyo
wa asilimia 50/50 wa faida.
Akifafanua
zaidi Dkt. Abbasi anasema kutokana na juhudi na mafanikio yaliyofikiwa na Serikali
ya Awamu ya Tano, Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD)
limeitaja Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika Mataifa ya Afrika Mashariki
kuvutia Wawekezaji kwa kuwa na mtaji wa Dola Bilioni 1.35 .
Dkt.
Abbasi aliwataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi na jitihada za Serikali
katika kuleta maendeleo, kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia
kuboresha na kuinua na kuboresha ustawi wa maisha ya wananchi wa hali ya chini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...