NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kuwa mkutano wa COP 23 ambao Mameya na watendaji wakuu wa majiji na miji mbalimbali duniani utatoa suluhisho la pamoja la kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi katika miji yao.

Akiwa Nchini Ujerumani , Meya Mwita emesema kuwa mkutano huo utakuwa mahususi kwa jiji la Dar es asalaam kupata suluhisho na kuhakikisha kuwa wanakabiliana ipasavyo na mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo janga la mafuriko ambalo limekuwa ni tatizo sugu jijini hapa.

Mkutano huo unaofanyika sambamba na Mkutano wa 23 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi, COP 23 inahusu miji na Taasisi zenye uhusiano na ubia na miji ya Ujerumani katika utekekezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko hayo inayofadhiliwa na Nchi hiyo.

Mkutano huo wa kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi umeandaliwa na Taasisi ya Engagement Global ya Ujerumani kwa miji washirika kutoka nchi mbalimbali duniani ambapo umeanza jana alasiri mjini Bonn nchini Ujerumani.

Kutoka Tanzania miji mingine inayoshiriki katika mkutano huo ni Jiji la Mwanza, Manispaa ya Zanzibar na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. 

Hata hivyo mkutano huo utaendelea hadi Novemba 11, mwaka huu ambapo jiji la Dar es Salaam linashiriki katika likiwa na ujumbe wake unao ongozwa na Mstahiki Meya Jiji hilo Mwita pamoja na Mkurugenzi Sipora Liana.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati mwenye koti jeusi , Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana wa kwanza kulia wakijadiliana jambo na ujumbe wa jiji la Hamburg katika mkutano wa mabadiliko ya Tabia ya Nchini unaoendelea Nchini Ujerumani.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati mwenye koti jeusi ,akiwa na Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana wakipata chai baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya mkuanomhuo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...