Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mshtakiwa Harbinder Singh Sethi,ameoimba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumruhusu kwenda kupatiwa matibabu ya puto lake lililoisha muda nchini Afrika Kusini kwa daktari wake maalumu kwa madai ya kwamba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamemueleza kuwa hawawezi kufanya upasuaji huo.

Maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo na wakili wake, Joseph Sungwa leo Novemba 10/2017 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, wakati shauri hilo linalomkabili Sethi na James Rugemarila lilipopelekwa kwa kutajwa na Mawakili wa Serikali, Vitalis Peter na Leonard Swai kudai upelelezi haujakamilika.

Katika kesi hiyo, Sethi na James Burchard Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kighushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Akiwasilisha maombi hayo, wakili Sungwa alidai alielezwa na mteja wake kwamba baada ya kufanyiwa vipimo na Muhimbili, walimweleza hawana ujuzi wa kumfanyia upasuaji wa puto.hilo na endapo litaendelea kubaki mwilini mwake linaweza kupasuka muda wowote na kuzalisha sumu ambayo litaatarisha maisha yake na njia pekee iliyobakia ni kwa mshtakiwa Sethi kumuona daktari wake anayeishi Afrika Kusini.

“Ili mshtakiwa aweze kuja mahakamani kuudhuria kesi yake na hatimae kuweza kujitetea, tunaomba kama inawezekana aende kumuona daktari wake ambaye anaishi Afrika Kusini kwa matibabu”, alidai Sungwa.

Ombi hilo lilipingwa vikali na wakili wa serikali,Swai akidai Muhimbili haijashindwa kumfanyia upasuaji wa puto mshitakiwa huyo, bali anajicheleweshwa mwenyewe kutokana na kutaka uwepo wa daktari wake wa Afrika Kusini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...