Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema litafikiria matumizi ya Boda boda na Bajaji kwa wageni watakao hitaji kutembelea Hifadhi zake endapo yatajitokeza maombi ya kutosha kuhusu matumizi ya vyombo hivyo.

Hatua hiyo inatokana na bidhaa mpya ya Utalii wa kutumia Baiskeli iliyoanzishwa hivi karibuni katika Hifadhi za Taifa za Mlima Kilimanjaro na Arusha kuanza kuwa kivutio kwa watalii kutoka nchi mbalimbali walioanza kufanya utalii wa Baiskeli.

Miongoni mwa watali hao ni pamoja na mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal aliyeweka rekodi ya kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.

Juanito na wenzake wawili , Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,wakianza safari yao kupitia lango la Kilema ,aina hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya katika Milima huo mrefu kuliko yote barani Afrika.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal aakiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia walipoianza safari ya kuelekea kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal akiwa katika kilele cha Uhuru mara baada ya kufanikiwa kufika huku akiendesha baiskeli . 
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal (katikati) akiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz(kushoto) na Ramon Abecia (Kulia) katika kilele cha Uhuru walipoanda kwa kutumia baiskeli .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadi za Taifa ,(TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza mara baada ya wageni hao kushuka baada ya kufanikiwa kufika kilele cha uHuru kwa kutumia Baiskeli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...