Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akizungumza
na Balozi mpya wa China nchini, Wang Ke, wakati balozi huyo alipomtembelea Masauni ofisini
kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati
ya China na Tanzania. Katikati ni msaidizi wa Balozi huyo, Liang Lin.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza
Balozi mpya wa China nchini, Wang Ke, wakati balozi huyo alipokua anafafanua jambo katika
mazungumzo yao yaliyofanyika katika ofisi ya Naibu Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walikubaliana kuendeleza ushirikiano zaidi kati ya
China na Tanzania. Katikati ni msaidizi wa Balozi huyo, Liang Lin.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkaribisha
ofisini kwake, Balozi mpya wa China nchini, Wang Ke (katikati), wakati balozi huyo
alipomtembelea Masauni ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadiliana
masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania. Kushoto ni msaidizi wa Balozi
huyo, Liang Lin. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...