NA RAMADHANI JUMA,OFISI YA MKURUGENZI

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amemaliza hofu ya kuhamishwa iliyokuwa imetanda kwa wafanyabiasha takribani 2,500 wa Soko la Sabasaba Mjini Dodoma baada ya kuwahakikishia kuwa wataendelea kufanya shughuli zao katika Soko hilo linalomilikiwa na Manispaa ya Dodoma na kwamba hakuna wa kuwahamisha.

Aliyasema hayo jana alipofanya ziara Sokoni hapo na kufanya mkutano na Wafanyabiashara hao ambao walimueleza Mkurungenzi huyo kuwa wamekuwa wakipata taarifa zisizo rasmi kuwa upo mpango wa wao kuhamishwa katika soko hilo hali inayowakosesha usingizi na kutojua hatma yao.

“Hakuna kuhama hapa ng’oo…Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ndiyo mmiliki wa Soko hili ambalo asili yake hapo awali lilikuwa eneo la Maonesho ya Sabasaba ambapo wadau mbalimbali walikuwa na vibanda vyao vya maenesho” alifafanua Kunambi huku akishangiliwa na wafayabiashara hao.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Kunambi alifuatana na Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede.Wafanyabiashara hao waliishukuru Manispaa ya Dodoma baada ya viongozi hao kufika na kuzungumza nao katika wakati muafaka baada ya kufanya biashara zao kwa wasiwasi mkubwa kwa siku kadhaa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba (hawapo pichani) Mjini Dodoma jana ambapo aliwahakikishia kuwa hawatahamishwa katika soko hilo. 
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya DodomaJumanne Ngede akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba Mjini Dodoma jana ambapo alifuatana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi. 
Sehemu ya Wafanyabiashara ya Manispaa ya Dodoma wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa Mkurugenzi huyo na wafayabiashara wa soko hilo jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...