Katibu wa Chadema mkoa wa Iringa Oscar Ndale katikati akiwa na diwani wa Mwangata Anjelus Mbogo na katibu kata ya Mwangata Tumaini Gwivaha baada ya kujiuzulu leo
Na MatukiodaimaBlog.
IDADI ya madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)
jimbo la Iringa mjini kujiuzulu imezidi kuongezeka na kufikia
madiwani saba sasa baada ya watatu kujiuzulu ndani ya wiki hii
pamoja na katibu wa chadema mkoa wa Iringa Oscar Ndale .
wakati diwani wa Kwakilosa na Ruaha walijiuzulu kwa pamoja juzi
diwani wa Mwangata Anjelus Mbogo alijiuzulu leo pamoja na katibu
wa mkoa wa chama hicho na katibu kata wa Chadema Mwangata
Tumaini Gwivaha .
wakitangaza azma ya kujiuzulu kwao nafasi hiyo mbele ya waandishi
wa habari Mbogo na Ndale walisema kuwa kujiuzulu kwao kumetokana na
mahusiano mabaya ya kufifisha maendeleo kwenye kata yake pamoja na mabavu ya viongozi w juu wa Chadema .
kati yake na viongozi wa
juu wa Chadema hicho akiwemo mwenyekiti wa kanda ya Nyasa Mchungaji
Peter Msigwa ambae ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini pamoja
na uongozi wa juu wa Chadema ukiongozwa na mwenyekiti wake Taifa
Freeman Mbowe.
" Vyama vya siasa vipo vingi kuna CUF , ACT Wazalendo na CCM
hivyo nitachagua ni chama gani kitanifaa kufanya siasa zangu ila
hata CCM nipo tayari hakuna ubaya "
Alisema kuwa mbunge Msigwa amekuwa akimfanyia diwani mwenzao
Joseph Lyata figisu figisu toka akiwa naibu meya wa Manispaa ya
Iringa na hofu ya
mbunge Msigwa ni baada ya kuhisi kuwa anautafuta ubunge wa jimbo
hilo mwaka 2020 .
Diwani Mbogo alisema kwa
sasa atabaki mwanasiasa huru na iwapo mbunge Msigwa na mstahiki
meya Alex Kimbe wataondoka hata leo chadema basi atarejea Chadema
ila kama wataendelea kubaki hatarudi kamwe .
Kwa
upande wake aliyekuwa katibu wa Chadema mkoa ,Ndale alisema kuwa
kuyumba kwa chadema Iringa mjini kumesababishwa na mbunge kutokuwa
na ushirikiano mzuri na wenzake na mara kadhaa wamekuwa wakimuonya
ila bado anaendelea na kuwa Mbowe pia amesababisha kujiuzulu
kwake nafasi hiyo na kwa sasa atajiunga na CCM .
Ndale
alisema aliomba kujiunga na CCM na amekubaliwa na hivyo ataendelea
na Siasa kupitia CCM huku akisema uhai wa Chadema Iringa mjini
umefika mwisho .
Kwa upande wake Joseph
Lyata aliyekuwa diwani kata ya Kwakilosa alisema siasa ndani ya
Chadema kwake imemshinda hivyo ameamua kuondoka ndani ya chama
hicho na kuwa mwanasiasa huru .
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini Omary Mkangama
ambae ni kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
amethibitisha kupokea barua za madiwani watatu ndani ya wiki hii
kutoka Chadema ambao wamejiuzulu nafasi zao Tandesy Sanga wa kata
ya Ruaha , Joseph Lyata kata ya Kwakilosa na Anjelus Mbogo wa kata ya
Mwangata .
"
Kwa mujibu wa sheria nitamuandikia barua mstahiki meya ili yeye
aweze kumwandikia waziri mwenye dhamana ambae ataijulisha tume
wa Taifa ya uchaguzi ili taratibu nyingine zifanyike "
Alisema
jimbo la Iringa linazo kata 18 kati ya madiwani hao CCM ina
madiwani watano pamoja na yule wa Kihesa aliyepita bila kupingwa
itakuwa na madiwani sita huku Chadema itabaki na madiwani 9.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...