Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa mbunge wa Kawe jijini Dar as Salaam, Halima Mdee aliitisha mkutano na waandishi wa habari ili kupinga kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo.
Ofisa wa Polisi, D/SSGT Arbogast ameyaeleza hayo leo,wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa baada ya kutupilia mbali kielelezo cha maelezo ya onyo kilichotolewa na upande wa mashtaka.
Akisoma uamuzi uliotupilia mbali kielelezo, Hakimu Nongwa amesema ametupilia mbali kielelezo cha upande wa mashtaka kwa sababu maelezo ya onyo ya mshtakiwa yalichukuliwa nje ya muda.
Akitoa ushahidi wake Arbogast amedai yenye ndiye aliyemfanyia mahojiano Mdee ambaye alikiri kuitisha mkutano na waandishi wa habari, July 3,mwaka 2017.Amedai mshtakiwa alimwambia ni kweli aliitisha mkutano na waandishi wa habari na lengo lake lilikuwa ni kupinga kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo.
Shahidi huyo amedai Mdee akiwa katika kituoni Oysterbay, July 8, mwaka jana na wakati akimhoji alimsikilizisha CD iliyokuwa na matamshi ya lugha ya fedheha dhidi ya Rais Magufuli.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 29, ambapo upande wa mashtaka utaendelea kuleta mashahidi.
Mdee anakabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha kwa Rais Magufuli, ambapo alitenda kosa hilo Julai 3,mwaka 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema imtaa wa Ufipa Kinondoni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...