Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Ibrahim Mussa a.k.a Roma Mkatoliki amefungiwa kwa kipindi cha miezi 6 baada ya kukaidi agizo la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) la kurekebisha wimbo wake wa Kibamia.
Roma aliitwa na BASATA baada ya agizo la Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Shonza la kumuita na kumtaka abadilishe maudhui ya wimbo wake unaojulikana kwa jina la Kibamia aliomshirikisha msanii mwingine Stamina na Maua Sama.
Agizo la kufungiwa kwa msanii Roma Mkatoliki limetoka leo kutoka BASATA linalosema kumfungia kwa kipindi cha miezi 6 kutokujihusisha na masuala ya muziki.
Wimbo wa Roma ulitoka takribani miezi mitatu iliyopita na alipoitwa BASATA alikiri wimbo kuwa na lugha isiyo nzuri na akaahidi kubadilisha maudhui ya wimbo huo ila muda umezidi kwenda bila kuufanyia marekebisho.
Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuufungia wimbo huo kutokupigwa katika vyombo vyote vya habari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...