Na Jumbe Ismailly, IKUNGI
IDADI ya wakazi wa vijiji vya Kaugeri na Mduguyu,kata ya Mwaru,wilaya ya Ikungi waliokosa makazi kutokana na nyumba zao kuanguka kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani hapa zimeongezeka kutoka kaya 22 zanye zaidi ya wakazi 154 hadi kufikia kaya 177 zenye zaidi ya wakazi 700 baada ya nyumba189 kuanguka.
Ongezeko la idadi hiyo ya wakazi linatokana na mvua kubwa iliyonyesha apr,16 hadi 18,mwaka huu na kusababisha mto kuacha njia yake na kulenga katika Kitongoji cha Mwasusu,na ndipo kaya 22 zenye zaidi ya wakazi 154 katika vijiji vya Kaugeri na Mduguyu,Kata ya Mwaru kukosa makazi baada ya nyumba 34 kuanguka.u
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mwaru,Hamisi Malongo alisema hayo alipokuwa akitoa taarifa za athari zilizotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa Mkoani Singida na kuongeza kwamba pamoja na nyumba hizo vile vile makanisa matatu ya FPCT na AIC yalianguka kufuatia mvua hizo.
“Na tuliloligundua sisi kama viongozi kama serikali upande wa kata kwamba vijiji vya Kaugeri na Mduguyu ni vijiji vya mpakani na Mkoa wa Tabora ambavyo ndiyo bonde la Mto Wembere unapita kwa hiyo mvua inaponyesha pande zote za dunia kwa hiyo wao ni rahisi sana kuathirika na mvua hizo.”alisisitiza Malongo.
Mmoja wa wananchi walioathirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha akiwa kwenye makazi yake mapya yaliyopo kitongoji cha Mwasusu,Kijiji cha Kaugeri akihofia wingu lililotanda kama alivyokutwa na kamera ya kituo hiki(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Baadhi ya wakazi wa vijiji vya Kaugeri na Mduguyu,kata ya Mwaru,wilayani Ikungi wakihamisha baadhdi ya vitu vilivyosalia kwenye makazi yao ya zamani na kuhamia kwenye eneo lililotengwa na serikali kwa ajili ya wahanga hao wa mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha kwa sisku tatu mfululizo na hivyo kusababisha zaidi ya wakazi 700 kukosa mahali pa kuishi
Ni Miundombinu ya barabara ya kutoka Mlandala kwenda kwenye Kitongoji cha Mwasusu,Kijiji cha Kaugeri sehemu iliyotengwa kwa ajili ya wahanga wa mafurriko ya mvua zilivyoharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Singida.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...