Ni baada ya mama Wema kudai mwanaye ameenda India kufanyia upasuaji

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuanza kusikiliza utetezi wa msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya sababu amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.

Taarifa hiyo imewasilishwa mahakamani hapo na Mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa Serikali, Constantine Kakula kuhoji kwanini Wema hakufika mahakamani.

Wakili Kakula alidai, kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya mshtakiwa Wema kuanza kujitetea lakini anashangaa kutokumuona mahakamani hapo kwani hata ahirisho la mwisho la kesi yake hakuwepo.

Kufuatia  hayo, Mama Wema alisimama na kutoa nyaraka za Wema za kusafiria na kuieleza mahakama kuwa Wema anaumwa na amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.

Wakili Kakula alidai hakuna uthibitisho wowote wa kuonesha Wema anaumwa, hivyo anaiomba Mahakama isimamie sheria.Kutokana na hoja hiyo, Hakimu Simba amesema ni kweli hakuna uthibitisho, hivyo katika tarehe ijayo uthibitisho unapaswa kuwepo, na kesi  imeahirishwa  hadi June 13 mwaka 2018.

Mbali na Wema, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni wafanyakazi wa Wema, Angelina Msigwa na Matrida Abbas. Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya.

Inadaiwa Februari 4 mwaka 2017 katika makazi ya Wema eneo la Kunduchi Ununio, washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa February Mosi mwaka 2017 katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...