NA TIGANYA VINCENT, TABORA

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, Uyui na maeneo mengine kuhakikisha wanasaidia kudhibiti uuzaji holela wa chakula unaofanywa na baadhi ya wananchi bila kujiwekea akiba kwa ajili ya siku za baadaye.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa kila familia iwe na akiba ya chakula ambacho kitaweza kuwafikisha  mavuno ya msimu ujao bila kuomba msaada Serikalini.

Mwanri ametoa kauli hiyo leo wilayani Uyui wakatika wa Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kinapitia mambo mbalimbali ikiwemo uhifadhi wa mazingira na chakula na kupitia taarifa za miradi mbalimbali.

Alisema utaratibu wa uuzaji wa chakula utakuwa kwa kila kaya kujaza fomu maalumu ambayo itaoonyesha chakula alichovuna msimu huu , matumizi yake kwa mwaka na ziada iliyobaki na ndipo ataweka sahihi ya kukiri taarifa kabla ya kuruhusiwa kuuza.

Mwanri alisema lengo la kufanya hivyo kutaka kuwabana wale wote wenye tabia ya kuuza ovyo ovyo chakula na kikiisha wanakimbilia kuomba msaada Serikalini wakati wenyewe ndio hawakuchukua tahadhari. Alisema pia mavuno ya mwaka huu kwa mahindi yanaweza yasiwe mazuri kutokana na mazao hayo kushambuliwa na wadudu , kwa hiyo ni vema watu wakachukua tahadhari mapema.

Mwanri alisema hamkatalii mtu kuuza mazao yake lakini akiwa Kiongozi wa Mkoa anabeba dhamana ya kuhakikisha usalama wa wananchi ukiwemo wa chakula ndio maana anataka atakayeuza awe kweli ana akiba ya kutosha ili isije ikafika wakati wa njaa anaandamana kwenda Mkoani kuomba msaada.

Kwa upande wa  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, Uyui, Said Ntahondi aliwataka Madiwani kuhakikisha wanasimamia maelekezo ya Mkuu wa Mkoa ya utunzaji wa chakula na kwa kushirikiana na Watendaji katika maeneo yao ili waweze kutoa taarifa ambazo ndio zitawapa fursa ya kukubaliwa kuuza au kutouza. Alisema mtu atakayeruhusiwa kuuuza chakula ni yule kweli ambaye anacho chakula cha kutosha familia yake kwa mwaka mzima na awe na ziada iliyothibitika.

Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Tabora , Uyui limekubalina kuwa kuanzia sasa kila familia lazima iwe na msitu wake na kila kijiji kiwe na msitu wake kama juhudi za kulinda mazingira. Ntahondi alisema hatua hiyo itasaidia katika kuhakikisha jamii inaanzakuwa na uwelewa mzuri kuhusu faida ya misitu na kukabiliana na wavamizi wa mistu.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora aliwaagiza Madiwani na Watendaji mbalimbali kuhakikisha wanasimamia Sheria katika kulinda hifadhi za mistu na vyanzo vya maji kwa ajili ya ustawi mzuri wa Mkoa huo.

Aliongeza kuwa katika maeneo ya miji  na barabara ambayo viti hajapandwa ni vema ikapanda ili kuipendezesha miji na kulinda mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...