Frank Mvungi- MAELEZO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amezindua Muongozo wa Tathmini ya Mazingira (SEA) ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kulinda mazingira ili yaweze kuchochea ukuaji wa uchumi na kuleta maendeleo endelevu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dodoma Waziri Makamba amesema kuwa dhamira ya Serikli ni kuhakikisha kuwa miradi yote mikubwa inayotekelezwa na Serikali pamoja na wawekezaji inafanyiwa tathmini hiyo ili kulinda mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.
"Nawapongeza WWF kwa kazi nzuri za tafiti wanazofanya na hata kupatikana kwa muongozo huu ni matokeo ya kazi nzuri waliyofanya kama wadau wetu ambao wamekuwa wanashiriki kikamilifu kuunga mkono juhudi za Serikali kulinda mazingira " Alisisitiza Mhe. Makamba
Akifafanua amesema kuwa anazikumbusha Wizara , Taasisi na wadau wote wanaotaka kutekeleza miradi ya maendeelo kuhakikisha kuwa wanazingatia muongozo huo ambao umekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inajenga uchumi wa viwanda.
Aliongeza kuwa Ofisi yake ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa SEA katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia washiriki wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa tathmini ya Mazingira Kimkakati Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa tathmini ya Mazingira Kimkakati Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Esther Makwaia akiwasilisha maelezo kuhusu muongozo wa tathmini ya Mazingira Kimkakati Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa tathmini ya Mazingira Kimkakati Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa hafla ya mwongozo wa tathmini ya Mazingira Kimkakati Jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...