Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarest Ndikilo akisalimiana na Wachezaji
wa timu ya Migomba kutoka Rufiji kabla ya kuanza kwa fainali ya kombe la
IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) iliyoikutanisha timu hiyo na Mjawa kutoka
Kibiti katika uwanja wa Samora Kibiti. Migomba walifanikiwa kutwaa
ubingwa baada ya kuichapa Mjawa penati 12 kwa 11.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarest Ndikilo akisalimiana na Wachezaji
wa timu ya Mjawa kutoka Kibiti kabla ya kuanza kwa fainali ya kombe la
IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) iliyoikutanisha timu hiyo na Migomba
kutoka Rufiji katika uwanja wa Samora Kibiti. Migomba walifanikiwa kutwaa
ubingwa baada ya kuichapa Mjawa penati 12 kwa 11.
Msanii Malima Ndolela akitumbuiza wakati wa sherehe za kufunga Michezo
ya kuwania kombe la IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) katika uwanja wa
Samora Kibiti. Timu ya Migomba kutoka Rufiji ililifanikiwa kutwaa ubingwa
baada ya kuichapa Mjawa penati 12 kwa 11.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Mrakibu Mwandamizi wa Polisi
(SSP) Chatanda akimkabidhi seti jezi nahodha wa timu ya Mjawa Bakari
Tuga kutoka Kibiti baada ya kushika nafasi ya pili katika kombe la IGP Sirro
(Sirro Cup 2018 Kibiti) iliyoikutanisha timu hiyo na Migomba kutoka Rufiji
katika uwanja wa Samora Kibiti. Migomba walifanikiwa kutwaa ubingwa
baada ya kuichapa Mjawa penati 12 kwa 11.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarest Ndikilo akimkabidhi kombe la
ushindi nahodha wa timu ya Migomba Maulid Mtupa baada ya kuibuka
mabingwa wa kombe la IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) kwa kuichapa
Mjawa kwa penati 12 kwa 11 katika uwanja wa Samora Kibiti. (Picha na
Jeshi la Polisi).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...