· Shindano la miezi mitatu lina lengo la kutoa elimu ya fedha na biashara kwa wamiliki wa biashara ndogo ndogo.
·
Benki ya FINCA Microfinance inaendelea kuwa benki ambayo inahamasisha
ushirikishwaji wa kifedha katika kipindi cha miaka 20 na zaidi ya uwepo
wake nchini Tanzania.
Tarehe
26 Juni, 2018 Dar es Salaam - Benki inayokua kwa kasi zaidi nchini
Tanzania, Benki ya FINCA Microfinance leo imetangaza uzinduzi wa
programu ya miezi mitatu na shindano ambalo linalengo la kuwaongezea
uwezo wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia stadi za biashara, ufahamu na
kisha kuwapatia zaidi ya TZS Millioni 10 kwa wazo bora la biashara
litakalokuwa limewasilishwa.
Shindano
linalojulikana kama 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika
katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na
Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko
Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa
Ndege.
Akiongea
wakati wa uzinduzi jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Masoko na
Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John alisema
kwamba lengo ni kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa
biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao,
Mshindi wa programu na shindano hili atawezeshwa kifedha kuendeleza
biashara zake ndogo ndogo ziliyopo.
"Shindano
hili litashirikisha wateja wa FINCA wenye akaunti na wale ambao
wanapenda kushiriki watatakiwa kufungua akaunti ya FINCA, ambao pia
watatakiwa kuweka kiasi cha TZS 20,000 (Salio jipya katika akaunti zao)
Watatakiwa kujaza fomu katika matawi ya FINCA ambapo watabainisha katika
fomu hizo kuwa wataenda kufanyia nini zawadi hiyo katika biashara zao
iwapo wataibuka kuwa washindi. Baada ya hapo fomu hizo zitawasilishwa
katika matawi yetu, mpaka hapo watakuwa wametimiza vigezo vya hatua ya
kwanza ya shindano".
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance, Nicholous John (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam. Kulia ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, Emmanuel Mongella na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba. Shindano la Kuza Ofisi na FINCA linalenga kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao. Mshindi wa programu na shindano hili atawezeshwa kifedha kuendeleza biashara zake ndogo ndogo ziliyopo.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, Emmanuel Mongella (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam.
Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba. Shindano la 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, mmanuel Mongella (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam.
Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba.
Shindano la 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...