Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAKALA wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini (TaGLA) wameendelea na mafunzo kwa njia ya mtandao kutoka Korea kusini kuhusiana na masuala ya utunzaji wa upangaji wa miji na utunzaji wa mazingira.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi wa Wakala hiyo Charles Senkondo ameeleza kuwa huo ni mdahalo wa pili kati ya saba inayotarajiwa kufanyika hadi kufikia oktoba mwaka huu, na mdahalo wa kwanza ulifanyika mapema mwezi huu na hii ni katika kujifunza jinsi ya kutunza mazingira na kupanga miji kisasa zaidi.

Senkondo ameeleza kuwa mafunzo hayo yanatolewa na profesa Heungsuk Choi kutoka chuo cha maendeleo cha korea kusini katika kueleza namna ya upangaji wa miji na majiji kisasa na kuzingatia usafi na miundombinu iliyo bora zaidi.Imeelezwa kuwa Korea Kusini ilikuwa sawa na Tanzania ya sasa katika miaka 1960 ila hadi sasa Korea kusini imepiga hatua kubwa sana hivyo kama wakala inajifunza hatua zilizochukuliwa katika uboreshaji wa miundombinu hiyo na usalama kwa ujumla.

Pia Senkondo amewaomba wadau wa serikali na taasisi binafsi kuitumia wakala hiyo ili kuweza kushirikiana na Serikali katika kujenga miji na kutunza mazingira.Naye mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche ameeleza kuwa wao kama taasisi ya serikali inayohusika na masuala ya mazingira semina hiyo inawasaidia sana katika uboreshaji wa mazingira na ulinzi hasa katika masuala ya usafi kwa kuzoa taka ili kuweza kupambana na magonjwa ya mlipuko sambamba na kuwa tayari katika kujipanga na mlipuko wa majanga kama mafuriko.

Aidha Manchare amesema kuwa changamoto kubwa katika suala la upangaji wa miji ni kutopanga mapema maeneo maalumu kama makazi na yale ya viwanda hivyo wamejipanga katika kulitatua hilo hasa katika jiji la Dodoma ambalo limekuwa makao makuu ya nchi.

Pia mdau wa mazingira ambaye pia ni mkurugenzi wa Legendary International Limited Kamugenyi Luteganya,  ameeleza kuwa semina hiyo ni muhimu sana katika jamii katika kuishi mazingira yaliyo bora na safi kama Korea wanavyofanya na kuboresha kwa kila hatua hivyo ni lazima wachukue ujuzi ili kuweza kuboresha makazi  nchini.
 Mwanasheria wa Mwandamizi (NEMC) Manchare Heche akichangia mada katika mkutano  wa mtandao uliofanyika jana jijini Dar,ambao ulihusisha nchi mbalimbali huku Nchi mwenyeji ikiwa ni Korea kusini 
 Mkurungenzi Mtendaji wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao,Charles  Senkondo akizungumza na waandishi wa habari  mbalimbali waliohudhuria mkutano wa mtandao uliohusisha nchi  mbalimbali ,mwenyeji ikiwa Nchi ya Korea kusini  jana  jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
 Mkutano wa mafunzo kwa njia ya mtandao ukiendelea, huku mada kuu ikiwa ni upangaji wa miji na majiji sambamba na utunzaji wa mazingira.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mjadala wa moja kwa moja kutoka Korea kusini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...