Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dk. Bashiru Ally amemtaka mfanyabiasha aliyetajwa kwa jina moja la Deogratius wa jijini hapa, kurejesha kwa hiari yake eneo la CCM ambalo anadaiwa kulihodhi kwa miaka kadhaa sasa katika Kata  ya Makutupola wilaya ya Dodoma Mjini ambalo amekujenga ukumbi na fremu kadhaa za maduka.
Dk. Bashiru ametoa agizo hilo kwa mfanya biashara huyo jana alipokuwa akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake katika Kata ya Nakutupola jijini hapa.Amesema amefikia uamuzi huo kwa sababu mfanyabiashara huyo ameonekana kutokuwa na uaminifu wa kutosha kwa kuwa hivi karibuni alizungumza nae ofisini kwake na kuahidi kukutana ili kufanya makabidhiano ya eneo hilo kwa sherehe na nderemo kwenye kikao hicho.

"Cha kushangaza juzi akikuja mwenyewe ofisini kwangu tukaxungumza kwa muda wa saa mbili tukakubaliana leo aje kwenye kikao hiki kukabidhi eneo letu kwa sherehe na ndelemo lakini leo nimempigia hadi simu akasema eti ameenda Dar es Salaam kushughulika na masuala ya mwanae, sasa  endeleeni na mazungumzo  na utaratibu wa makabidhiano akabidhi kwa hiari eneo letu", alisema Dk Bashiru

Dk. Bashiru aliwataka wanachama na viongozi wa CCM kutofanya vurugu za aina yoyote kwa Mfanya biashara huyo na kusema Mchakato uliotumika kurejesha ukumbi ndio utakaotumika kurejesha eneo lote la  Chama na mali yote iliyopo kwenye eneo la hilo ni mali ya CCM.

Katika mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally amewapokea Winston Edward Katibu Kata hiyo wa CUF na Baraka Tayara Katibu kata wa Chadema pamoja na wanachama 181 kutoka vyama hivyo. Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally akipokelewa na Viongozi mbali mbali alipowasili kata ya Makutupola wilaya ya Dodoma mjini jana Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akiwapungia Mkono kikundi cha ngoma Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akizungumza na Viongozi na wanachama wa CCM na Jumuiya zake wa Kata ya Makutupola jana.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...