SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wamekabidhi rasmi kijiji cha digitali cha Ololosokwan katika sherehe kubwa iliyofanyika kijijini hapo na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Katika kukabidhiana huko Unesco imesema kwamba itaendelea kutoa msaada katika mtandao wa intaneti kwa miezi sita ijayo.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Dk. Abdul Rahman Lamin, Ofisa msimamizi wa ofisi ya Unesco, Ann Therese Ndong-Jatta alisema kwamba wakati wanakabidhi facility hizo wamefurahishwa na ushirikiano mkubwa waliopewa katika mradi huo.

Kijiji cha digitali cha Ololosokwan ni moja ya vijiji vinne ambavyo vimefadhiliwa huku vikitoa huduma muhimu za elimu, afya na biashara kuendeshwa kidigitali.Kijiji hicho cha digitali ambacho ni matokeo ya ushirikiano kati ya UNESCO na kampuni ya Samsung imelenga kutoa elimu kwa kutumia njia ya mtandao, kufaniklisha tiba mtandao na pia kutumia mtandao wa kompyuta katika kuwezesha biashara.

Ofisa huyo alisema kuna haja ya kuendeleza ushirikiano uliopo ili mradi uweze kuendelea kuchangia maendeleo ya wakazi wa eneo hilo.
Aidha aliitaka serikali kuhakikisha kwamba inaendeleza ushawishi kwa wananchi wa eneo hilo la Ngorongoro kutumia vyema teknolojia ya kisasa katika kufanikisha maisha endelevu ya zana zilizopo.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo akizungumza na wananachi wa kijiji cha Ololosokwan pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Abudl Rahman Lamin (wa tatu kushoto) akimwakilisha Ann Therese Ndong’ Jatta, Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki akimkabidhi rasmi ripoti ya mradi wa kijiji cha kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mh. Rashid Mfaume Taka (wa tatu kulia) kwa ajili ya uendelezaji baada ya majaribio wakati wa hafla iliyofanyika katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni cha jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. 

Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria Semakafu (waliosimama kwa nyuma), Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo (kushoto), Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi (wa pili kushoto), Diwani wa kata ya Ololosokwan, Mh. Yannick Ndoinyo (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ololosokwan, John Pyando (kulia).
 Baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan waliohudhuria hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

HABARI ZAIDI BOFYA  HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...