Na Agness Francis, Globu ya Jamii
KLABU Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC imetangaza rasmi kuwa imemsajili kiungo Tafadzwa Kutinyu mkataba wa mwaka mmoja.
Kiungo huyo atachezea kikosi cha Azam FC ambacho maskani yake iko Chamazi jijini Dar es Salaam. Mchezaji huyo amekuwa na msimu mzuri tokea ajiunge na Singinda United msimu huu ambaye alitokea katika klabu ya Chicken Inn ya nchini kwao Zimbabwe.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa Azam FC Jaffary Iddy amesema mchezaji huyo ambaye mkataba wake uko wazi ni mapendekezo ya mwalimu Hans Van Der Pluijm raia wa Ubolanzi.
"Tunaamini mwalimu anamfahamu vizuri ndio maana amemuhitaji.Pia tutaangalia maandeleo yake mchezaji huyo anaisaidiaje timu,akiwa anafanya vizuri basi tutamuongezea mkataba mnono zaidi" amesema na kuongeza kuwa Kutinyu atavaa rasmi uzi wa Azam katika mashindano ya CECAFA ambayo timu hiyo ndiye mtetezi wa Kombe hilo.
"Tutarejea tena kuutetea ubingwa wetu baada ya mashindano hayo kusimama kwa muda wa miaka 3 bila kufanyika"amesema Jaffary.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...