Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba wanawake wenye tabia ya kuvaa sketi fupi maarufu Vimini na nguo za kubana wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan wakaacha kuzivaa katika kipindi hiki ili kuhakikisha waumini wa dini ya Kiislamu wanatekeleza funga hiyo vema.
Makonda ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anapokea msaada wa tende kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi Darul Irshad Centre Islamic Tanzania Arif Yusuf AbduRahman kwa kushirikiana na taasisi rafiki ya Muraj Islamic Centre Tanzania.Makonda ameagiza tende hizo zipelekwe katika vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Wakati anazungumzia funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambayo waumini wa dini ya Kiislamu wanaendelea nayo amesema ni vema waumini wa dini zote wakashiriki katika kufanikisha waliofunga wanatekeleza moja ya nguzo za dini hiyo vema.Hivyo amewaomba wanawake wenye tabia ya kuvaa vimini na nguo za kubana katika mwezi huu wakaacha kuzivaa ili kutoa nafasi ya waliofunga kutoingia majaribuni kutokana na mavazi hayo.
"Niwaombe akina dada wanaopenda kuvaa nguo za kubana hasa vimini kuacha kuvaa hadi hapo mfungo utakapokwisha.Natambua wananchi wa Mkoa wa Dar es Salam wapo wenye imani tofauti lakini bado tunayo nafasi ya kuheshimi imani ya kila mmoja wetu,"amefafanua Makonda.Pia ametoa ombi kwa wafanyabishara kutopandisha bei ya vyakula katika kipindi ambacho waumini wa dini ya Kiislamu wanaendelea na mfungo wa mwezi wa Ramadhan.
"Wananchi wa Dar es Salaam niendelee kutoa ombi tuwape ushirikiano ndugu zetu walioko kwenye funga na kwa wafanyabiashara msipandishe bei ya vyakula,"amesisitiza.Kuhusu tende ambazo zimetolewa na taasisi hiyo Makonda amesema zitakwenda kugawiwa vituo vya watoto yatima vilivyopo Dar es Salaam na anaamini kwa kugawa tende hizo kwenye vituo hivyo ni sehemu ya kuwakumbuka watoto walioko huko ambao wapo ambao wapo kwenye funga.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Taasisi ya Darul Irshad Centre Islamic Tanzania wakibeba tende kabla kukabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Taasisi ya Darul Irshad Centre Islamic Tanzania wakibeba tende kabla kukabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Darul Irshad Centre Islamic Tanzania AbduRahman leo jijini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...