RAIS wa awamu ya tatu wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa anataraji kuwasili nchini mapema kesho kwa ziara ya siku mbili kuanzia June 28 hadi 29 mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametangaza leo.
RC Makonda ameeleza kuwa Mnangagwa atapokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere na mwenyeji wake Rais John Magufuli majira ya saa tano kamili asubuhi.
RC Makonda ameeleza kuwa Mnangagwa atapokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere na mwenyeji wake Rais John Magufuli majira ya saa tano kamili asubuhi.
Amesemqa kuwa ujio huo wa Rais wa Zimbabwe una lengo kuu ambalo ni kudumumisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya Tanzania na Zimbabwe tangu wakati wa kupigania uhuru wa taifa hili la kusini mwa Afrika.
Makonda amesema kwamba Mnangagwa ataondoka nchini june 29 asubuhi akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Magufuli na ametoa wito kwa wakazi wa Dar es salaam kumkaribisha mgeni na wageni wote waingiao nchini kwa kuwafanya wajisikie wako nyumbani kwa muda wote watakaokuwa jijini.
Ikumbukwe kuwa hii ni ziara ya kwanza ya Rais Mnangagwa wa Zimbabwe kufika nchini Tanzania tangu alipoingia madarakani Novemba 2017.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu ziara ya kikazi ya Rais wa Zimbabwe Mh. Emerson Mnangagwa.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...