MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ,Moshi imeelezwa upelelezi wa shauri la mauaji linalomkabili mmiliki wa shule ya sekondari ya Scolastica umekamilika.

Wakili wa serikali anayeiwakilisha Jamhuri katika shauri hilo, Agatha Pima aliieleza mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo la mauaji ya kukusudia ya mwanafunzi Humphrey Makundi umekamilika kwa asilimia 100.

Baada ya maelezo hayo,wakili wa upande wa utetezi anayemtetea mtuhumiwa wa pili katika shauli hilo,Edward Shayo,Elikunda Kipoko aliwasilisha ombi mbele ya mahakama hiyo kutoa kibali cha kuruhusu mteja wake kupatiwa matibabu kutokana na ugonjwa unaomsumbua.Hata hivyo ombi hilo lilikataliwa na Hakimu Mkazi Wilaya ya Moshi,Julieth Mawole akieleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa kibali kwa mtuhumiwa huyo.

Hakimu Mawole ameeleza kuwa kila mtu ana haki ya msingi ya kupatiwa matibabu lakini mahakama hiyo haina mamalaka ya kutoa kibali kwa mtuhumiwa huyo na kwamba suala hilo liko Magereza.Aidha Mawole alieleza kuwa mchakato wa kuhamisha jalada la kesi ya mauaji kwenda mahakama kuu utafanyika June,29 mwaka huu.

Hatua ya upelelezi kukamilika unafikiwa baada ya watuhumiwa hao kukaa rumande kwa zaidi ya miezi saba wakati wakiendelea kusubiri kukamilika kwa upelelezi huo.Shauri hilo la mauaji ya kukusudia linawakabili, mmiliki wa shule ya Sekondari ya Scholastica pamoja mlinzi wa shule hiyo,Hamis Chacha na mwalimu wa shule hiyo Laban Nabiswa .

Mnamo Novemba 6,mwaka jana Mwanafunzi huyo ,mwili wake ulikutwa umetupwa mto Ghona mita 300 kutoka eneo la shule hiyo ambapo mwili huo ulizikwa katika makaburi ya Manispaa ya Moshi Novemba 12,mwaka jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...