Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Wakulima wazidi kuneemeka kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.

HALMASHAURI ya Wilaya Kibiti imezidi kuwaneemesha wakulima wa ufuta kutokana na bei ya mnada kupanda ni baada ya serikali kuagiza zao hilo kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani na kufanya wakulima kunufaika na kilimo hichio.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Gulamhussein Kifu wakati wa mnada wa tano wa zao la Ufuta katika wilaya hiyo amesema kuwa mnada huo ni wa tano na bei bado imekuwa ikiongezeka kutoka 2750 katika mnada wa kwanza hadi kufikia sh.3115 katika mnada wa tano kwa kilo moja ya Ufuta.

Amesema kuwa licha ya kuwa mnada kuwa mzuri kwa wakulima wanatakiwa kuhifadhi Ufuta bora ili wafanyabiashara bidhaa bora.Kifu amesema kuwa wakulima wataopatikana kutia doa pamoja na vyama ushirika hawataacha salama.

Amesema mnada huo ukiharibiwa na watu wachache kwa makusudi binafsi kutafanya wafanyabiashara wakimbie soko.Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Alvera Ndabagoye katika minada Mitano wa wameuza kilo zaiidi ya Milioni 1.6. 

Amesema mafanikio hayo ni dhahiri kuwa uzalishaji wa ufuta utaongezeka katika msimu ujao ,kwani wakulima walikata tamaa kutokana na bei ndogo waliyokuwa wakiuza kwa walanguzi.Aidha amesema kuwa baadhi ya wakulima kupeleka ufuta katika maghala bila kuusafisha na kusababisha malalamiko kwa wafanyabiashara.

"Kitendo cha kupeleka ufuta bila kusafisha ni makosa na tabia hiyo iachwe mara moja na kila mkulima asafishe ufuta wake"amesema Ndabagoye.Amesema chama chochote cha msingi au mkulima wataobainika kupeleka ufuta bila kusafisha watachukuliwa hatua za kisheria pamoja na kufunga ghala husika.
 .Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Gulamhussein Kifu akihutubia katika mnada huo uliofanyiaka katika ofisi ya mkuwa wilaya.
 Watuza funguo Afisa Ushirika wa Wilaya na Mwenyekiti wa AMCOS ya Kibiti wakifungua sanduku la tenda.
Baadhi ya wafanyabiashara, wakulima na watumishi waliohudhuria mnada huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...