NA WAMJJW-DAR ES SALAAM
WIZARA ya afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imetangaza rasmi kuanzia Juali 1 2018 imepokea Hospitali 28 za Rufaa za Mikoa ambazo zilikuwa chini ya usimamizi wa OR-TAMISEMI .
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala. “Hospitali ambazo tumezipokea zina jumla ya vitanda 7,474 na jumla ya watumishi 8,671 ambao, kati yao Wauguzi ni 3,960, Madaktari 536, Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali ni 182, na waliobakia ni watumishi wa kada zingine mbalimbali za Afya” alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ambazo Wizara imezipokea ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru (Arusha), Dodoma General (Dodoma), Kitete (Tabora), Shinyanga, Geita, Singida, Mpanda (Katavi), Mawenzi (Kilimanjaro), Bombo (Tanga), Morogoro, Ligula (Mtwara), Sokoine (Lindi), Maweni (Kigoma), Sekou Toure (Mwanza), Mwananyamala, Amana, Temeke (Dar es Salaam), Songwe, Kibena (Njombe), Iringa, Tumbi (Pwani), Sumbawanga (Rukwa), Bariadi (Simiyu), Musoma (Mara), Songea (Ruvuma), Mbeya, Babati (Manyara) na Bukoba (Kagera).
Waziri Ummy alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2018/19, Wizara imetenga shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya kipaumbele katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ambako tayari huduma zinatolewa ikiwemo Matibabu kwa wagonjwa wa dharura ,Huduma za upasuaji wa dharura hususan wakati wa ujauzito na uzazi pamoja na Huduma za tiba kwa wagonjwa mahututi zikiwemo za watoto wachanga .
Mbali na hayo Waziri Ummy amesikitishwa na upungufu wa wodi pamoja na vitanda kwa ajili ya wanawake wanaofika kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala na kuahidi kulifanyia kazi mara moja iwezekanavo. “Kama Mama,na nimeumia sana na lazima tulifanyie ufumbuzi mara moja kwahiyo namuagiza katibu mkuu alete mtaalamu wa majengo na tupandishe fedha za kujenga ghorofa mbili mara moja kwakweli halii hii haikubaliki” alisema Waziri Ummy.
Mnamo Novemba 25, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizindua Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) aliagiza kuwa Hospitali za Rufaa za Mikoa zihamishiwe kwenye usimamizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJW) kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akitoa maelekezo juu ya matangazo yaliyo kwenye mbao mapema leo wakati
alipofanya ziara ya kukagua huduma za Afya zinazotolewa katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akimsikiliza moja kati ya wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa ya Mwananyamala wakati alipofanya ziara mapema leo katika
Hospitali hiyo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akimsikiliza kwa makini Bi Halima Said aliyefika kupata huduma za
matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala pindi
alipofanya ziara mapema leo katika Hospitali hiyo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akiongea na Bi. Angelina Erasto juu ya umuhimu wa kukata Bima ya Afya ya
TOTO AFYA KADI itakayomsaidia kupunguza gharama za matibabu kwa mtoto
wake
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akishangaa idadi kubwa ya wakina mama iliyozidi kiasi katika wodi ya
kupumzikia wakina mama baada ya kujifungua, akiwa katika ziara yake ya
kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala kukagua ubora wa
Huduma zitolewazo katika Hospitali hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...