Na Zainab Nyamka Globu ya Jamii
TIMU ya soka ya Lipuli FC ya mkoani Iringa jana imekamilisha  usajili wa wachezaji wake wapya wanne kutoka timu tofauti ili kuongeza nguvu kwenye msimu wa 2018/19.

 Lipuli wameweza kuwapata  nyota wawili waliowahi kukipiga klabu ya Simba pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Yanga , Paul John Nonga kutoka Mwadui FC ya Shinyanga aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja.

Usajili umewahusisha beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, William Lucian ‘Gallas’ kutoka Ndanda FC ya Mtwara na mshambuliaji Miraj Madenge ‘Shevchenko’ kutoka Mwadui FC ambao wote kila mmoja amesaini mkataba wa mwaka mmoja pamoja na Issa Ally Rashid, mchezaji huru ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili. 

Gallas na Miraji waliwahi kukipiga katika klabu ya Simba kuanzia timu ya Vijana  kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2013 na baadaye kuchwa mwaka 2014.

Lipuli iliyoanza vizuri msimu wake wa kwanza ndani ya ligi kuu vodacom wakiwa chini ya kocha Selemani Matola  imedhamiria kufanya vizuri msimu kwa kufanya usajili utakaokuwa na tija na kuleta ushindani ndani ya ligi.
Beki William Lucian 'Gallas' akipokea kandarasi yake ya mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Lipuli Fc ya Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...