Na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha.

Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ameeleza kuwa Serikali inatambua juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kutangaza utamaduni wa Mtanzania pamoja na kukuza soko la ajira kupitia kazi za sanaa nchini.

Hayo ameyasema leo Jijini Arusha , alipokuwa akifungua Tamasha la TANZANIA MAMA NI WATHAMANI “TAMANI FESTIVAL” ASANTE MAMA 2018 lililoandaliwa na Tanzania Gospal Nertwork Artist (TAGOANE ) lenye lengo la kulinda na kuendeleza utu wa mwanamke.

“Naipongeza timu nzima ya TAGOANE kwa juhudi kubwa walioifanya katika kujenga misingi imara ya utamaduni wa kumuwezesha, kumuendeleza na kulinda UTU wa mwanamke kwa ustawi wa taifa letu ” amesema Mhe. Juliana Shonza.Aidha Mhe. Shonza aliongeza kwa kueleza kuwa Wizara kupitia Idara ya Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa itashirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali katika kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ambapo kwa sasa sanaa imekuwa kiwanda kinachozalisha ajira kwa wingi.

Alizidi kufafanua kuwa Tamasha la TAMANI FESTIVAL ni kichochea kikubwa katika kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya sanaa, ubunifu na ujasiriamali hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kuweza kushiriki katika kuonyesha bidhaa zao.Naye Rais wa Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network Dkt. Godwin Maimu ameeleza kuwa uongozi wa taasisis hiyo utahakikisha unatangaza na kuhubiri maadili mema na kuhimiza uzalendo kwa vijana ili kuwa na jamii bora yenye kuleta maendeleo.

Tamasha la TAMANI FESTIVAl limefanyika kwa mara ya kwanza na kuzinduliwa katika Jiji la Arusha , ambapo baadaye wamedhamilia kuendelea kulitambulisha katika mikoa mingine ya Tanzania
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na wadau wa Sanaa na Utamaduni ( hawapo katika Picha), wakati wa ufunguzi wa tamasha la TAMANI FESTIVAL lililopewa jina la TANZANIA MAMA NI WA THAMANI ASANTE MAMA 2018, chini ya uratibu wa Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE) Jijini Arusha.
Rais wa Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network(TAGOANE) Dkt. Godwin Maimu akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Hayupo katika picha), wakati wa ufunguzi wa TAMANI FESTIVAL Jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Kushoto) akisalimiana na Mjasiriamali wa bidhaa za chupa za urembo Bibi . Glory Silayo (kulia) anayemiliki kampuni ya AfricanBae, katika uzinduzi wa TAMANI FESTIVAL Jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na wakina mama wa jamii ya kimasai waliohudhuria uzinduzi wa TAMANI FESTIVAL katia viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisikiliza maelekezo ya namna ya kumsaidia mtu aliyepata ajali kutoka kwa Mkufunzi wa Huduma ya Kwanza wa Msalaba Mwekundu Bw. Tisian Temba (kulia) katika uzinduzi wa TAMANI FESTIVAL Jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akipimwa presha na Muuguzi Mkuu Mwandamizi kutoka Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru Bibi. Patricia Khatibu , alipotembelea banda hilo wakati wa uzinduzi wa TAMANI FESTIVAL lililoandaliwa na Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha,(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...