Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola
akizungumza katika kikao chake na Maafisa Waandamizi wa Idara ya Uhamiaji
kuhusu utaratibu wa kuunganisha mifumo ya vibali vya kazi na ukaazi. Kulia ni Kaimu
Kamishna wa Vibali vya Ukaazi, Idara ya Uhamiaji, Mary Palmer, kushoto ni Afisa
wa Kitengo cha Vibali vya Ukaazi, Isaac Fota, pamoja na Afisa Mahafudhi
Nassoro. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo,
jijini Dodoma leo, kabla ya kikao chake na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto
meza kuu), akimsikiliza Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,
Jenista Mhagama alipokua akifafanua jambo kuhusiana na mfumo unaoziunganisha
Wizara hizo mbili, wa utoaji wa vibali vya kazi na ukaazi. Kikao hicho kilifanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, jijini Dodoma leo. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola
akizungumza katika kikao cha kujadili mfumo wa pamoja wa utoaji wa vibali vya
kazi na ukaazi. Kulia meza kuu ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Jenista Mhagama. Mfumo huo unaoziunganisha wizara hizo mbili. Kikao
hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya wa Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Walemavu, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiwa
ofisini kwake jijini Dodoma mara baada ya kuwasili jijini humo leo. Waziri
Lugola alifanya kikao na Maafisa Uhamiaji kutoka Kitengo cha Vibali vya Ukaazi,
na baadaye alifanya kikao na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Jenista Mhagama jijini humo, wakijadili mfumo wa pamoja wa utoaji wa
vibali vya kazi na ukaazi ambao unaziunganisha Wizara hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akikaribishwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, ofisini kwake jijini Dodoma, kabla ya Mawaziri hao kuanza kikao cha kujadili mfumo wa pamoja wa utoaji wa vibali vya kazi na ukaazi ambao unaunganisha wizara hizo mbili. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, jijini humo leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...