Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii

MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)kwa kushirikiana na Taasisi ya mafunzo ya masoko ya Mitaji na uwekezaji (CISI) wamezindua mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa washiriki wa masoko ya mitaji nchini, (CPD).

Ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati ya kuwajengea uwezo na kuimarisha ufanisi kwa watendaji na wataalamu wanaishiriki katika mitaji ili kufikia viwango vya ubora wa kimataifa,
(EASRA).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo jijini Dar es Salaam Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama amesema,    mpango huo unaweka utaratibu na vigezo vya ushiriki kwa washiriki wa masoko ya mitaji kufikia angalau masaa 10 ya ushiriki wa mafunzo ya masoko ya mitaji kwa mwaka.

Na kuwa hiyo itakuwa kigezo kimojawapo cha utoaji wa lesebi ya ushiriki katika masoko ya mitaji ifikapo Januari mwaka 2020.

Ameongeza kuwa washiriki wa masoko ya mitaji walio na leseni watatakiwa kufanya mafunzo na kutekeleza mipango inayotambuliwa na CMSA na CISI katika kutekeleza vigezo vya mpango wa mafunzo endelevu na kupewa idhini itakayotolewa kwa taarifa maalumu itayowasilishwa CMSA kwa ajili ya taarifa na kuweka kumbukumbu.

" Mpango wa mafunzo endelevu utawawezesha watendaji ndani ya masoko ya mitaji kutoa huduma kwa umahiri mkubwa zaidi kwa kuendana na maendeleo yanayotokea katika masoko ya mitaji duniani,"amesema Mkama na kuongeza.

"Ushirikiano kati ya Mamlaka ya taasisi ya CISI unayaweka masoko ya mitaji ya Tanzania katika ramani ya masoko ya mitaji ya dunia kwa kuwa na wataalamu wanaokidhi viwango vhhya kimataifa," amesema.

Kwa upande wa Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya CMSA, Emmanuel Kakwezi kwa niaba ya mwenyekiti, ameitaka mamlaka kuhakikisha inakuwa na wataalamu wa kutosha katika masoko ya mitaji wanajiunga na mpango huo ili kulinda uwezo wa kitaaluma na uhalali wao katika ulimwengu wa ushindani.

Amesema masoko ya mitaji ni sekta inayobadilika kwa kasi na yenye kuhusisha viashiria vya aina mbali mbali,

Wakati huo huo Mkurugenzi wa DCSI, Kevin Moore ushirikiano huo utawawezesha watanzania kuongeza uwezo wa kuelewa kwa nji ya mitandao na hata ile njia halisi.

Pia amesema mafunzo hayo endelevu yatasaidia wataalamu na kuifanya Tanzania kuendelea kuongeza ufanisi katika soko la kimataifa.
   Mjumbe wa Bodi  ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Masoko ya mitaji na dhamana, Emmanuel Kakwezi akisoma taarifa yake kuashiria uzinduzi wa mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa washiriki wa masoko ya mitaji nchini, (CPD).
Mkurugenzi wa CISI,  Kevin Moore akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa washiriki wa masoko ya mitaji nchini, (CPD).
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama akielezea umuhimu wa wa mpango wa ushirikiano wa CMSA na CISI kwa washiriki wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa washiriki wa masoko ya mitaji nchini, (CPD).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...