NA MWAMVUA MWINYI,VIGWAZA
DIWANI
wa kata ya Vigwaza ,Bagamoyo , Pwani ,Mohsin Bharwani (CCM),amechangia
mabati 242, mifuko ya saruji 100 na matofali 3,000 vyenye thamani
takriban sh.milioni 12 katika kijiji cha Chamakweza,Mnindi na kitongoji
cha Serengeti.
Amesema
ametoa vifaa hivyo vya ujenzi ,ili kutekeleza ilani ya CCM na kuunga
mkono juhudi za wananchi katika miradi wanayoiibua na miradi ya
serikali.Bharwani
alitoa michango hiyo, katika ziara yake ya kutembelea baadhi ya miradi
ya maendeleo katika vijiji vilivyopo kata ya Vigwaza ,ambapo ameanza
kwenye vijiji vya Chamakweza,Mnindi na kitongoji cha Serengeti.
"Shule ya msingi Chamakweza ambayo darasa moja na ofisi havina mabati nimetoa mabati 96 yenye thamani ya sh.milioni 2.8 " #"Katika
kitongoji cha Serengeti kilio cha wananchi ni kupata shule ya awali ,na
tunashukuru halmashauri imeleta mshauri kutoka idara ya elimu msingi
kwenye mkutano huu kwani tumepata nafasi ya kumueleza adhma yetu na
kutupa maelekezo" alifafanua .
Kutokana
na hilo ,Bharwani alitoa ,mifuko ya saruji 50 ,matofali 2,000 ,licha ya
kuendelea kwa hatua nyingine zitakazozingatia vigezo vinavyotakiwa ili
kufikia hatua ya kupata kibali cha kujenga na kuwa na shule si tu ya
awali bali shule ya msingi.Akiwa
kijiji cha Mnindi ambacho kinaendelea na ujenzi wa zahanati alisema
,"wakati ujenzi ulipoanza alichangia mifuko 50 na kwasasa amechangia
mabati 96 yenye thamani ya milioni 2.8.
"Serikali
inafanya mambo makubwa kwa utkeleza miradi mbalimbali ya reli
,barabara,umeme,afya,elimu na maji hivyo lazima viongozi wa chini tuunge
mkono juhudi hizo ,na kushirikiana na rais Dk.John Magufuli kutatua
kero mbalimbali kuanzia ngazi ya chini ""Rais
karudisha imani kwa wananchi na wadau wanaoshiriki kusaidia masuala
mbalimbali, katupa jeuri CCM kutokana na kutekeleza ahadi na ilani kwa
kugusa kila eneo ili kuinua maendeleo na uchumi ." alisema Bharwani.
Bharwani
aliwataka ,viongozi wa kuchaguliwa na watendaji wengine kuunganisha
nguvu na ya wananchi kuisaidia serikali ya CCM ili kipiga hatua zaidi
wakati nchi ikielekea kwenye uchumi wa kati .Akizungumza
kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ,Erasto Meshack kutoka idara ya
elimu msingi alisema ,kwa mujibu wa miongozo kigezo cha kwanza ili shule
iitwe shule inapaswa kujengwa katika eneo lisilozidi hekari kumi . .
Alieleza ,ili shule iweze kufunguliwa isipungue majengo sita,stoo,vyoo vya walimu ,wanafunzi na nyumba za walimu.Nae
,mwenyekiti wa kijiji cha Vigwaza Ramadhani Kirumbi, alimshukuru diwani
huyo kwa michango yake anayojitolea ,kwani kutoa ni moyo .Alisema
endapo mradi wa ujenzi wa shule ya awali ya Sekibwa kitongoji cha
Serengeti ukifanikiwa utawasaidia watoto ambao hutembea zaidi ya km.tano
kufuata elimu hiyo nje ya eneo hilo .Mwenyekit wa CCM kata ya Vigwaza
,Shederi Mkole ,alimpongeza Bharwani kwa kujitoa kwake kutekeleza ilani
ya CCM.
DIWANI wa kata ya Vigwaza , Mkoani Pwani ,Mohsin Bharwani (CCM),akizungumza katika kijiji cha Chamakweza wakati alipofanya ziara yake katika kijiji hicho ,kijiji cha Mnindi na kitongoji cha Serengeti.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkazi wa Chamakweza ,Philemon Molel akimshukuru diwani wa kata ya Vigwaza ,Mohsin Bharwani wakati alipokwenda kutembelea miradi na kijijini hapo ,kijiji cha Mnindi na kitongoji cha Serengeti. (Picha na Mwamvua Mwinyi).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...