Na Mary Gwera, Mahakama
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amewasihi Watumishi wa Mahakama kuwa na utayari katika matumizi ya mifumo mbalimbali ya Teknolojia inayoanzishwa Mahakamani ili kuendelea kuboresha huduma ya utoaji haki nchini.
Aliyasema hayo Agosti 02, alipokuwa akiwasilishiwa mada juu ya mfumo wa ‘Video Conferencing’ utakavyofungwa na utakavyofanya kazi katika Mahakama husika iliyowasilishwa na Mkandarasi atakayefanya kazi ya ufungaji wa mfumo wa ‘Video Conferencing’, Kampuni ya ‘Invention Technologies.’
“Mahakama yenyewe inatakiwa kuwa tayari kutumia mifumo mbalimbali inayowekwa ili hata Wadau wengine kama Magereza, Polisi waweze kwenda sambasamba na Mahakama katika kuboresha huduma ya utoaji haki,” alisisitiza Mhe. Feleshi.
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akiongoza majadiliano mara baada ya uwasilishwaji wa mada ya mfumo wa ‘Video Conferencing.’
Wajumbe wakifuatilia mada katika kikao hicho.
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akiongea jambo katika kikao hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...