Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa amemtaka Mkandarasi anayejenga Daraja la Magara linalounganisha Wilaya ya Babati na Mbulu kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ujenzi wake unakamilika kwa haraka na ubora unaotakiwa ili kuwaondolea wananchi kero ya usafiri inayowakabili.

Akizungumza mara baada ya kukagua daraja hilo, Kwandikwa amesema tayari kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kimelipwa kama malipo ya awali hivyo Mkandarasi aongeze kasi na kulimaliza daraja hilo pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa Kilomita 4.9 katika kipindi cha miezi 24.

“Daraja hili likikamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa litahamasisha shughuli za biashara na uzalishaji kati ya Mbulu na Babati na hivyo kuchochea uchumi wa wilaya hizo” amesema Kwandikwa.Aidha amemtaka Mkandarasi China Railway Seventh Group (CRSG) anaejenga daraja hilo kutoa fursa za ajira kwa wakazi wa Wilaya za Mbulu na Babati katika kuharakisha ujenzi wake.

Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Manyara, Mhandisi Bashiri Rwesingisa amemhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kuwa ujenzi wa Daraja la Magala ni Sehemu ya Mkakati wa Serikali wa kuijenga barabara ya Kutoka Mbuyu wa Mjerumani hadi Mbulu kwa Lami ambapo tayari upembuzi yakinifu kwa ajil ya ujenzi huo umekamilika.
Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Manyara, Mhandisi Bashiri Rwesingisa akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (aliyevaa kofia) kuhusu hatua iliyofikia ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Mizani ya kudumu katika eneo la Mwada-Mbuyu wa Mjerumani, Wilayani Babati. Mkoani Manyara.
Muonekano wa mto Manyara ambapo linajengwa daraja la Magara lenye urefu wa mita 84, wilayani Babati Mkoani Manyara. Daraja hilo linatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 24.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Manyara kuhusu kuzingatia viwango katika ukarabati wa barabara sehemu ya mlima Magara kwa kiwango cha zege mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Mkoani Manyara.
Mafundi wakindelea na ujenzi wa barabara sehemu ya Magara kwa kiwango cha zege, Mkoani Manyara.
Muonekano wa barabara Magara-Mbulu ambayo inafanyiwa ukarabati na Wakala wa Barabara Nchini (TNAROADS) kwa kiwango cha zege,Mkoani Manyara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...