Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WANAFUNZI wa shule mbalimbali za Sekondari nchini wamekutana na kuonesha mawazo yao ya kiugunduzi kupitia taasisi ya Young Scientist (YS) na kuiomba Serikali kuwasaidia ili kufanikiwa katika kutimiza ndoto zao.

Katika hali ya kushangaza na kuvutia zaidi wanafunzi wa shule ya sekondari Vingunguti jijini Dar es salaam walionesha mazingaombwe kama vile kupoteza na kuirudisha sarafu, kujitoboa sehemu za miili yao na kudhibitisha kwamba dhana ya mazingaombwe ni sayansi na si usihiri (uchawi) kama inavyofahamika na watu wengi.

Akizungumza na Michuzi blogu mmoja wa wanafunzi hao Neema Julius ameeleza kuwa jamii itambue kuwa mazingaombwe ni sayansi inayotumika kila siku katika mazingira yetu na kwa utafiti wao wamegundua hakuna dhana ya ushirikina katika hilo.

Aidha wanafunzi kutoka shule ya sekondari Same wamegundua umeme wa utokanao na mitetemo, sauti na upepo na wameona umeme huo utafaa katika maeneo ya vijijini kwani changamoto zake ni chache ila kutokana na vifaa na uwekezaji wameiomba serikali kutoa msaada ili waweze kukamilisha ndoto zao za kuwasaidia wananchi kupata nishati ya umeme.

Pia shule ya Sekondari ya Mtakatifu Joseph Kolping baada ya kuona ongezeko la ajali za barabari wakaona watafute mbinu ya kudhibiti na wakaja na dhana ya matumizi ya roboti kuwa mlinzi na mwongozaji wa watumiaji wa barabara na kuripoti kila aina ya kosa linalotendeka.
 Mwanzilishi mwenza wa YST, Dr. Gosbert Kamugisha akipata maelezo kuhusu matumizi ya umeme wa upepo, sauti, na mtetemo kutoka kwa mwanafunzi wa Same Sekondari, Samwel Osebius.
 Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya mtakatifu Joseph Kolping, Fransisco Solomon akionesha roboti waliyoitengeneza kwa ajili ya kulinda  barabarani.
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Vingunguti, Neema Julius akieleza namna mazingaombwe yana uhalisia wa sayansi tofauti na wanajamii wanavyofikiri.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...