Watumishi wa Wakala wa Huduma Tanzania (TFS) wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na sheria za utumishi wa Umma ili kuleta ufanisi wakati wanapotekeleza majukumu yao ya uhifadhi.
Rai hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati alipowatembelea jana watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kanda ya Kusini kwa ajili ya kuzungumza nao ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii.
Amewataka kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu na yeyote atakayetuhumiwa kupokea rushwa hata kama hajapokea rushwa hiyo kutoka wafugaji kwa makubaliano ya kuingiza mifugo hifadhini kwa makubaliano ya malipo atashughulikiwa ipasavyo.Aliongeza kuwa endapo watumishi hao wataweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo hakuna kiongozi yeyote watakayesumbuana nao.
‘’Tunataka mfanye kazi zenu za uhifadhi kwa weledi wa hali ya juu na mkifanya vizuri basi nakuwa nimefanya mimi na mkifanya vibaya mnakuwa mnaniangusha mimi hivyo sitokubali’’ alisisitiza Naibu Waziri Hasunga.
Aidha, Amewata wafanye kazi kwa kushirikiana na jamii kwa vile hakuna shughuli yeyote itakayofanikiwa endapo wananchi wataachwa nyuma.
‘’Tunataka jamii ione faida ya moja kwa moja kwa kupata elimu kuhusu uhifadhi pamoja na kushirikishwa kwenye masuala yote ya misitu ili waweze kutoa ushirikiano wakati ukataji miti unapofanyika popote pale’’
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na
Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) wa kanda ya
Kusini, Ebramtino Mgiye mara baada ya kuwasili jana kwenye ofisi za TFS
kanda ya Kusini kwa ajili ya kuzungumza nao ikiwa ni muendelezo ya ziara
yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia
changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na
watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) wakati
alipowatembelea jana kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini ikiwa ni
muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa
ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji
Utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga(katikakati) akiwa
kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na Watumishi wa Wakala
wa Huduma za Misitu Tanzania kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini ikiwa
ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa
ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji
Utalii.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...