Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MSEMAJI wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakaluka amesema mbwa anayedaiwa kupotea hakuwa amepotea bali alikuwa katika mafunzo.

Amesema mbwa huyo alikuwa katika bwalo akiendelea na mafunzo na hivyo amewaomba Watanzania kufahamu hakuna mbwa aliyepotea.

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu leo jijini Dar es Salaam Mwakaluka amefafanua mbwa anayedaiwa kupotea yupo kwenye mikono salama ya Jeshi la Polisi na kwamba yupo kwenye mafunzo.

Amefafanua kuwa wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo Ndani alipokwenda bandarini hakumkuta mbwa hiyo hivyo baadhi ya waandishi wakadhano amepotea lakini ukweli ni kwamba alikuwa mafunzoni.

"Mbwa yupo kwenye mikono salama na yupo kwenye mafunzo,habari ya kwamba mbwa ameonekana Kenya si kweli," amefafanua.Alipoulizwa mbwa huyo alikuwa katika mafunzo ya aina gani,Mwakaluka amejibu hawezo kuelezea aina ya mafunzo ambayo amepewa kwani hayo ni mambo ya kitaaluma na ni kwa ajili ya Polisi.

Kuhusu cheo cha mbwa huyo amesema hana cheo bali ni mbwa mwenye mafunzo ya polisi na wameamua kutoa ufafanuzi huo ili umma ujue kuwa mbwa yupo na wala hajapotea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...