Na Rhoda Ezekiel Kigoma. 

TATIZO la Wazazi kutelekeza watoto Wilayani Kakonko Mkoani kigoma limekuwa sugu jambo ambalo linapelekea watoto wengi kukosa haki yao ya kupata elimu kama watoto wengine.

Akizungumza Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule ya Msingi Churazo ,Silvia Mgina, alisema tangu mwaka 2014 hadi sasa wamepokea watoto 128 waliotelekezwa na wazazi wao na kushindwa kupelekwa shule; hata hivyo kwa sasa wamekwisha waandikisha watoto hao.

Hayo yalibainika jana wakati wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi katika jimbo la Buyungu, baada ya Mbunge wa jimbo la Nzega mjini Hussein Bashe alipobaini kuwepo na watoto watatu katika Kijiji cha Churazo Wilayani humo,January Magaruka (13), Erick Magaruka (11),John Magaruka (9) waliotelekezwa na wazazi wao na kulelewa na Askari Mgambo katika Kijiji hicho.

Ambapo aliwachukua watoto hao na kuwakabidhi kwa Mbunge wa Vijana wa Mkoa wa kigoma , Zainabu Katimba na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo kuomba wawalee watoto hao na kuhakikisha wanapata elimu na malezi bora ." Nikienda katika mikutano ya kampeni huwa napenda kuzungumza na watoto ili kujua matatizo waliyonayo. 
 
Na nimebaini watoto kadhaa Wilayani Kakonko wamekimbiwa na wazazi wao na wengine wanaishi katika mazingira magumu, jamii na viongozi wa Wilaya hii wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kuhakikisha watoto wa aina hii wanapatiwa elimu", alisema Bashe.
 Mbunge wa jimbo la Nzega mjini Hussein Bashe na Mbunge wa Viti maalumu wa vijana Mkoani Kigoma Zainabu Katimba, akikabidhi fedha za kuwanunulia nguo za shule za watoto waliotelekezwa na Wazazi wao kwa mwalimu Mkuu msaidizi Silvia Mgina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...